![]()  | 
| Jengo la Chuo Kikuu Dodoma(Udom) moja ya vyuo vitakavyo tumika katika utaratibu huo mpya | 
Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.
Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 
2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la 
saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi
 ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na
 Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani
 mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu 
kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya 
kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, 
lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha
 mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama 
‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa 
vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.
Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya 
Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk 
Maronga na kuongeza:
“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini 
wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa 
habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo 
bila tatizo.”
Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 
75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja
 E ni 0-34.
“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa 
kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa 
kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha 
kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.
SOURSE: MWANANCHI
SOURSE: MWANANCHI
