
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
 wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo na Seneta, 
James Inhofe wa Jimbo la Oklahoma, wakati alipomtembelea Ofisini kwake 
baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Seneta huyo Feb 
6, 2013. Makamu wa Rais yupo nchini Marekani katika jiji la Washngton Dc
 kwa ziara ya siku nne.

Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
 akizungumza na Naibu Waziri wa Uchumi, Nishati na Mazingira, 
Seneta,Robert D. Hormats, wakati alipofika katika Ofisi yake iliyopo 
katika jingo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa katika ziara yake 
ya siku nne katika jiji la Washngton Dc Marekani, Feb 6, 2013.

Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
 akisalimiana na Balozi Johnnie Carson, wakati makamu alipofika Ofisini 
kwa Balozi huyo kwa mazungumzo, Feb 7, 2013. Balozi Carson ni 
msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala 
ya Afrika.

Makamu wa Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, 
akiagana na Rais wa Mfuko wa MCC, Daniel Yohannes, baada ya kumalizika 
kwa mazungumzo yao kuhusu kuendelea kwa mradi wa MCC ii, nchini Tanznia.
 Mazungumzo hayo yalifanyika jana Feb 6, 2013 katika Hoteli ya Omni 
iliyopo Washngton Dc Marekani, ambapo Makamu yupo nchini humo kwa ziara 
ya siku nne. Picha na OMR