Kiwanda
 cha ChemiCotex kilichopo huko Africana njia ya Tegeta jijini Dar es 
Salaam kimeungua moto jioni ya leo tar 30/01/2013.
Pages
▼
Wednesday, January 30, 2013
IGP MWEMA APATA AJALI MBAYA MOROGORO
IGP SAID MWEMA
Jinamizi
 la ajali  limeendelea  kuwaandama viongozi  wa  juu  serikali na vyama 
baada ya  juzi waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kunusurika kifo katika
 ajali  iliyotokea eneo la Bwawani mkoani Morogoro  ,Mkuu  wa jeshi la 
polisi nchini (IGP )  Said Mwema leo amenusurika  kifo  baada ya gari 
lake  alilokuwa akisafiria  kupinduka.
Ajali 
 hiyo  imetokea  majira ya mchana katika  eneo Mkundi Manispaa ya 
Morogoro wakati kiongozi huyo akitokea  jijini Dar es Salaam kwenda 
mkoani Dodoma.
Hata 
 hivyo katika ajali  hiyo hakuna madhara makubwa kwa  binadamu zaidi ya 
gari  kuharibika  kiasi na msafara  wa  IGP kuendelea na safari  ya 
Dodoma kwa  kutumia usafiri mwingine .






