Sentahafu wa Zambia Stopilla Sunzu amechukua likizo fupi kutoka kwenye kambi ya timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2013 ili apate nafasi ya kwenda nchini England kwenda kufanya vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo.
Sunzu ambaye anachezea klabu ya TP Mazembe ya DRCambayo imeandika kwenye mtandao wake kwamba ada ya uhamisho ya $4.8million imeshakubaliwa na kilichobakia ni mchezaji kukamilisha vipimo vya afya.
Mfungaji huyo wa penati ya ushindi ya Zambia dhidi ya Ivory Coast katika AFCON 2012, anatarajia kurudi Afrika ya kusini January 19, siku mbili kabla ya mabingwa watetezi kuchuana na Ethiopia katika mechi ya ufunguzi.
Sakata la mchezaji wa kimataifa wa
Uganda anayeichezea klabu bingwa ya Tanzania Bara Simba SC, Emmanuel
Okwi kwenda kujiunga na kambi ya Simba iliyopo nchini Oman limefikia
mwisho. Kwa taarifa za ndani kutoka ndani ya
klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo imefikia maamuzi ya kumuuza
mshambuliaji huyo kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho
itakayovunja rekodi ya uhamisho hapa nchini ya $300,000. Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Simba Mh.
Aden Rage kwa sasa yupo nchini Tunisia akisimamia taratibu zote za
uuzwaji wa Okwi ambaye alisaini mkataba mpya wa kuitumikia Simba hivi
karibuni. "Ni kweli Mwenyekiti yupo Tunisia
akishughulikia uuzwaji wa Okwi kwa klabu ya Etoile du Sahel. Ada ya
uhamisho ni dola laki tatu na muda mchache ujao dili litakamilika na
Okwi atapewa ruhusa ya kuzungumza maslahi binafsi na klabu yake mpya." -
kilisema chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba.
Etoile du Sahel ni klabu mojawapo yenye
mafanikio makubwa barani Afrika, ikiwa inashikilia rekodi ya kuwa klabu
pekee barani afrika kushinda kila kombe linaloandaliwa na CAF.